×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Kiambaa, Paul Koinange unazikwa Jumanos

Mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Kiambaa, Paul Koinange unazikwa Jumanos

Watu wasiozidi hamsini ndio pekee wanaotarajiwa kuhudhuria hafla ya mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Kiambaa, Paul Koinange leo hii kuambatana na masharti ya serikali ya kudhibiti kusambaa kwa virusi vya korona.

Ibada ya wafu itafanyika Katika Kanisa la St. John Kiambaa kuanzia mwendo wa saa tano asubuhi na itachukua tu saa moja huku Rais Uhuru Kenyatta akitarajiwa kuwa miongoni mwa watakaoudhuria.

Kisha itafuata hafla ya mazishi itakayohudhuriwa na watu wachache ambao ni familia nyumbani kwake katika eneo la Kiambaa. Peter Mwathi ni Mwenyekiti wa Kamati Andalizi ya Mazishi ambaye pia ni Mbunge wa Limuru.

Koinange alifariki dunia siku ya Jumatano alipokuwa  akitibiwa katika Narobi Hospital baada ya kuugua COVID-19.

Kabla ya kifo chake alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Usalama.

Share this: