×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Hospitali ya Mater yaachilia mwili wa Prisicilla Oendo

Hospitali ya Mater yaachilia mwili wa Prisicilla Oendo

Hatimaye Hospitali ya Mater imeiruhusu familia moja kuchukua mwili wa mpendwa wao uliokuwa umezuiliwa kufuatia deni.

Famila ya marehemu, Prisicilla Oendo ikiongozwa na mumewe William Nyambuti iliruhusiwa kuuchukua mwili huo hapo jana kufuatia uamuzi wa Hakimu P.O Muholi baada ya familia kunyimwa mwili huo kwa zaidi ya miezi miwili sasa kufuatia deni.

Priscillah aliaga dunia tarehe 8 Januari akiwa na deni la shilingi milioni  5.5 baada ya familia kulipa shilingi milioni 1.4 ambazo ni sehemu ya shilingi milioni 7 zilizohitajika.

Baadaye,  familia ilifanya mchango na kukusanya shilingi milioni 2 zaidi na kufikisha nusu kiwango cha fedha kilichohitajika lakini hospitali ikaendelea kukatalia mwili ikitaka fedha zote zilipwe.

Kufuatia hatua ya Hospitali ya Mater kuendelea kukatalia mwili,  familia hiyo kupitia wakili Benjamin Bogonko ilielekea mahakamani na hakimu  P.O Muholi kuitikia wito wao kwamba ikabidhiwe mwili.

Kwa mujibu wa jamaa ya mwendazake Isaac Ondeyo, Hospitali ya Mater ilikubali kuikabidi familia mwili huo jana jioni baada ya kupokea agizo la mahakama na familia hiyo ilifanikiwa kuuhamisha hadi Hifadhi ya Maiti ya Umash huku mipango ya mazishi ikiendelea.

Share this: