×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Wakenya wapunguziwe kodi wakati huu wa korona, asema Karua

Wakenya wapunguziwe kodi wakati huu wa korona, asema Karua

Kinara wa NARC Kenya, Martha Karua ni kiongozi wa hivi punde kushinikiza serikali kuwapunguzia Wakenya kodi wakati huu taifa linapokumbwa na wimbi la tatu la korona.

Kupitia mtandao wake wa Twitter, Karua amesema Wakenya hasa wafanyabiashara wanapitia hali ngumu ya maisha hasa kwenye kaunti tano zilizofungwa kwa muda ili kuepuka maambukizi zaidi.

Karua amesema biashara kwenye kaunti za Nairobi, Kiambu, Kajiado, Machakos na Nakuru zimeathirika pakubwa hasa ikizingatiwa tayari baadhi zimefungwa na wafanyakazi kutumwa nyumbani.

Kauli yake inajiri wakati ambapo Gavana wa Machakos, Alfred Mutua tayari amewapunguzia wafanyabiashara kodi wanazotozwa kila mwezi. Aidha, Mutua aliagiza maduka makuu kuwapunguzia wakazi bei za bidhaa.

Share this: