×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Kibwana atangaza mabadiliko katika Baraza la Mawaziri

Kibwana atangaza mabadiliko katika Baraza la Mawaziri

Gavana wa Makueni Kivutha Kibwana amefanya mabadiliko katika Baraza lake la Mawaziri ambapo ameeleza kuwa amefanya hivyo kuboresha utoaji huduma Makueni.

Aliyekuwa Waziri wa Kilimo na Unyunyiziaji, Robert Kisyula amehamishiwa Wizara ya Jinsia, Watoto na Masuala ya Kijamii, naye  Lawrence Nzung'a aliyekuwa akihudumu katika wizara hiyo kuhamishiwa ile ya  Biashara na Viwanda.

Aliyekuwa Afisa Mkuu wa Wafanyakazi wa Makueni, Nzioki King'ola sasa ndiye Waziri wa Kilimo ambapo jina lake limewasilishwa bungeni kabla ya kufanyiwa mchujo.

 Urbanas Mutinda Mativa aliyekuwa msaidizi wa Mbunge wa Kibwezi Magharibi, Patrick Musimba ameteuliwa kuwa Mshauri wa Gavana Kibwana. Katibu wa Kaunti ameshauriwa kuhakikisha mabadiliko hayo yanatekelezwa bila matatizo yoyote.

Share this: