×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Odinga hajatuma maombi ya kuwania urais 2022

Odinga hajatuma maombi ya kuwania urais 2022

Chama cha ODM sasa kinadai kuwa taarifa ilichotuma katika vyombo vya habari kwamba Kinara wake Raila Odinga amewasilisha stakabadhi za kutafuta tiketi ya kupeperusha bendera ya ODM, ilikuwa si ya kweli.

Kulingana na taarifa nyingine leo hii ambayo imetumwa na Katibu Mkuu wa ODM Edwin Sifuna, ilikuwa njama ya Fools Day, kwani walifahamu watu hasa wanasiasa watalichangamkia tangazo hilo n.

Sifuna amesema washindani wa kisiasa wa ODM walipata fursa ya kuzungumzia tangazo hilo na hawakufahamu halikuwa la kweli.

Sifuna amesema Odinga hakutuma ombi la kutaka kupeperusha bendera hiyo ya ODM, akisema waliotumua tu ni Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho na Mwenzake wa Kakamega Wycliff Oparanya.

Katika taarifa ya jana Sifuna alisema Odinga angekabiliana na wawili hao na kuwa stakabadhi zao maombi zilikuwa zimewasilishwa katika Bodi ya Uchaguzi ya ODM.

Makataa ya kutuma maombi hayo yalikamilika hapo jana.

Ikumbukwe awali Raila alisema kwamba hatazungumzia masuala ya uchaguzi wa mwaka 2022, akisema anasubiri hadi baada ya kukamilika kwa mpango wa BBI.

Share this: