×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Watu 1064 waambukizwa korona, 185 wapona, 7 wafariki

Watu 1064 waambukizwa korona, 185 wapona, 7 wafariki

Kwa mara nyingine Waziri wa Afya, mutahi Kagwe amesisitiza kwamba Chanjo ya Oxford/AstraZeneca ni salama kwa matumizi ya binadamu.

Kagwe aidha, amewaondolea Wakenya hofu hasa baada ya baadhi ya mataifa ya Bara Uropa kusitisha kwa muda utoaji wa chanjo hiyo kufuatia madai kwamba inasababisha mgando wa damu.

Kagwe sasa amewasihi Wakenya kujitokeza ili kuchanjwa dhidi ya virusi hivyo. Amerejelea kauli kwamba yu tayari kuchanjwa atakapotakiwa kufanya hivyo.

Wakati uo huo, Afisa Mkuu Mtendaji wa Idara ya Utafiti na Sayansi katika Shirika la Afya Duniani, WHO Soumya Swaminathan ameyataka mataifa kuendelea kutumia chanjo hiyo.

Haya yanajiri huku viwango vya maambukizi nchini vikiongezeka hata zaidi na kufikia asilimia 17.3 kulinganishwa na asilimia 16.2 ya jana.

Viwango vya leo vimeripotiwa baada ya watu wengine elfu moja, sitini na wanne kuambukizwa virusi hivyo leo hii. Idadi ya leo imetokana na sampuli elfu moja, mia moja hamsini na moja zilizopimwa katika saa 24 zilizopita.

Kagwe pia amethibitisha kupona kwa wagonjwa mia moja themanini na watano. Idadi hii inafikisha jumla ya waliopona kuwa elfu themanini na nane, mia saba themanini na mmoja.

Kulingana na Kagwe, idadi ya vifo imefikia elfu moja, mia tisa ishirini na vitano baada ya watu wengine saba kufariki.

Wakati uo huo, wagonjwa 709 wamelazwa katika hospitali mbalimbali nchini, elfu mbili mia mbili ishirini na watatu wanahudumiwa nyumbani.

Aidha, wagonjwa 104 wako katika vyumba vya wagonjwa mahututi, 25 wanatumia vipumuzi, 70 wanatumia oksijeni, 9 wakihitaji uangalizi wa karibu yaani HDU.

Share this: