×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Awamu ya kwanza ya chanjo ya Covid-19 kuwasili leo siku.

Awamu ya kwanza ya chanjo ya Covid-19 kuwasili leo siku.

Awamu ya kwanza ya dozi ya chanjo milioni nne ya ugonjwa wa Covid-19 ya Oxford/AstraZeneca inatarajiwa kuwasili humu nchini kesho.

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe alitarajiwa kuzuru Bohari ya Kitengela kukagua mikakati ya kuihifadhi chanjo hiyo kabla ya ziara hiyo kuahirishwa.

Serikali inaendelea kuboresha mikakati ya kuhakikisha kuwa Wakenya milioni 1.75 wanapewa kinga hiyo katika awamu ya kwanza ambayo itafanyika kati ya Machi na Juni mwaka huu.

Awamu ya pili itawalenga watu milioni 9.7 kati ya Julai mwaka huu na Juni mwaka 2022 na awamu ya tatu ikiwalenga takriban watu  milioni 4.9

Chanjo ya AstraZeneca inahitaji kuhifadhiwa katika sehemu yenye kiwango cha kati ya nyuzi joto mbili hadi nane.

Chanjo hiyo italetwa nchini kupitia mpango wa Umoja wa Mataifa kwa Ushirikiano na Shirika la Afya Duniani WHO na COVAX.

Mataifa mengine ya Afrika ambayo yamepokea chanjo kupitia COVAX ni Ghana na Ivory Coast huku Nigeria ikitarajiwa kupokea chanjo yake Jumanne hii sawa na Kenya.

Share this: