×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

OPDD yasema ina ushahidi mpya katika kesi ya uhalifu wa kiuchumi inayomkabili Gavana Korane

OPDD yasema ina ushahidi mpya katika kesi ya uhalifu wa kiuchumi inayomkabili Gavana Korane

Mkurugenzi wa Mashkata ya Umma, DPP Noordin Haji sasa anasema ofisi yake ina ushahidi mpya katika kesi ambapo Gavana wa Garissa, Ali Korone na maafisa wanne wa kaunti hiyo wanatuhumiwa kufuatia ufisadi.

Kesi hiyo ambayo ilipaswa kusikilizwa leo hii imesitishwa hadi tarehe 19 Aprili mwaka huu kuruhusu Upande wa Mashtaka kuwasilisha ushahidi huo.

Mbele ya Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Milimani, Douglas Ogoti DPP amepewa siku kumi na nne kuwasilisha ushahidi huo.

Aidha, ametoa makataa ya siku kumi na nne nyingine ili kuruhusu upande wa utetezi kujiandaa kwa kesi hiyo.

Mwezi Septemba mwaka uliopita, Korane alizuiliwa kuiangia ofisini hadi pale kesi dhidi yake itakaposikilizwa na kuamuliwa.

Gavana Korane anatuhumiwa kufuatia utakatishaji wa fedha money laundering, takriban shilingi milioni 233 za Benki ya Dunia.

Korane na washtakiwa wengine wanne tayari walifunguliwa mashtaka ya kujaribu kuiba fedha hizo. Hata hivyo, walikana mashtaka dhidi yao mbele ya Hakimu Ogoti.

Share this: