×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

KNUT yaitaka serikali kuwaongeza walimu mishahara

KNUT yaitaka serikali kuwaongeza walimu mishahara

Chama cha Kitaifa cha Walimu, KNUT kimetaka Tume ya Huduma za Walimu, TSC kuwaongezea walimu mishahara kuanzia mwezi Julai mwaka huu.

Katibu Mkuu wa chama hicho, Wilson Sossion amesema ni sharti TSC itii mkataba wa makubaliano hasa ikizingatiwa Tume ya Kuratibu Mishahara ya Wafanyakazi wa Umma, SRC imeidhinisha kwamba walimu waongezewe mishahara.

Aidha, viongozi wa chama hicho tawi la Bonde la Ufa wametishia kufanywa kwa mgomo iwapo mkataba huo hautazingatiwa.

Aidha, viongozi hao wameitaka serikali kukoma kumhangaisha Sossion.

Wakati uo huo, Mwakilishi wa Kike wa kwanza wa KNUT tawi la Kibwezi, Mercy Kyambati ameitaka TSC kukoma kuwashurutisha walimu kuhudhuria mafunzo ya Mtalaa wa Umilisi, CBS wikendi.

Share this: