
Kenya itapokea chanjo dhidi ya Korona Jumanne wiki hii. Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema kwamba watakaokuwa wa kwanza kupewa chanjo hiyo ni wahudumu wa afya.
Ikumbukwe awali Waziri Kagwe alitangaza kwamba Kenya itapokea dozi milioni nne za chanjo ya Oxford/AstraZeneca kupitia mpango wa Umoja wa Mataifa kwa Ushirikiano na Shirika la Afya Duniani WHO COVAX.
Mpango wa COVAX ndio unaotumika kusambaza chanjo kwa mataifa ya Afrika kwa kuzingatia idadi takwimu yaani; idadai ya watu walioambukizwa, waliopona na waliofariki dunia.
Katika mpango wa awali Wizara ya Afya ilitangaza kwamba chanjo itatolewa kwa awamu tatu ambapo katika awamu ya kwanza watu milioni 2.5 watachanjwa kati ya Machi na Juni mwaka huu. Awamu ya pili itawaelnga watu milioni 9.7 kati ya Julai mwaka huu na Juni mwaka 2022 na awamu ya tatu ikiwalenga takriban watu 4.9
Mataifa mengine ya Afrika ambayo yamepokea chanjo kupitia COVAX ni Ghana na Ivory Coast huku Nigeria ikitarajiwa kupokea chanjo yake Jumanne pia.
Share this: