×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Watu wengine 325 waambukizwa virusi vya korona

Watu wengine 325 waambukizwa virusi vya korona

Kiwango cha maambukizi ya virusi vya korona kimeanza tena kuongezeka leo hii kikiwa asilimia 10, kulinganishwa na jana ambapo kilikuwa asilimia 3.2.

Kiwango hiki kimetokana na kuambukizwa kwa watu wengine 325 kutoka kwa sampuli elfu 3,282.

Idadi hii sasa inafikisha watu elfu mia moja na tano, mia tisa sabini na watatu idadi ya jumla ya maambukizi nchini. Katika maambukizi hayo Kaunti ya Nairobi inaendelea kuongoza kwa kuwa na watu wengine 207 walioambukizwa viruis hivyo hatari.

Katika taarifa kwenye vyombo vya habari, Wizara ya Afya imesema wagonjwa 347 wa Covid-19 wamelezwa kwenye hospitali mbalimbali huku elfu 1,495 wakihudumiwa nyumbani. Aidha mgonjwa mmoja anahitaji uangalizi wa karibu.

Takimu hizo aidha zinaonesha kwamba wagonjwa wengine 69 wamepona ambapo 58 walikuwa wakihudumiwa nyumbani, 11 wakiwa wale waliokuwa wakihudumiwa hospitalini. Kwa jumla waliopona sasa ni elfu themanini na sita, mia sita sabini na wanane.

Wakati uo huo wagonjwa wengine wawili wamefariki dunia kutokana na makali ya Covid-19  na kufikisha jumla ya walioaga kuwa elfu moja, mia nane hamsini na sita.

Share this: