×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

ODM imejondoa katika uchaguzi mdogo kwenye wadi za London na Hells Gate, Kaunti ya Nakuru.

ODM imejondoa katika uchaguzi mdogo kwenye wadi za London na Hells Gate, Kaunti ya Nakuru.

Chama cha ODM leo kimejondoa katika kinyanganyiro cha uchaguzi mdogo kwenye wadi za London na Hells Gate katika Kaunti ya Nakuru.

Mwenyekiti wa ODM tawi la Nakuru Peter Gikaria imesema badala yake itaunga Jubilee mkono katika uchaguzi huo mdogo.

Kuondoka kwa ODM katika uchaguzi huo mdogo kunamaanisha kwamba ushindani mkali utakuwa baina ya Jubilee na UDA.

Chama cha UDA ambacho nembo yake ni wilbaro kilimkabidhi bendera Anthony Wachira Nzuki katika wadi ya London naye Jonathan Warothe huko Hells Gate.

Anthony Wachira ndiye mgombea wa UDA katika wadi ya London huku Jonathan Warothe akitarajiw akupeperusha bendera hiyo katika wadi  ya Hells Gate.

Ikumbukwe mwezi Disemba mwaka jana, Jubilee ilijiondoa katika kinyang'anyiro cha uchaguzi mdogo a Eneo Bunge la Msambweni, katika Kaunti ya Kwale na kumuunga mkono mgombea wa ODM Omar Boga.

Hata hivyo Boga alibwagwa na aliyekuwa mgombea binafsi Feisal Badar aliyeungwa mkono na Naibu wa Rais William Ruto.

Jubilee aidha ilijiondoa katika uchaguzi mdogo wa Kibra mwezi Novemba 2019 na kumuunga mkono mgombea wa ODM Imran Okoth ambaye alimshinda mgombea wa Ruto McDonald Mariga. 

Share this: