×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Sitaendeleza kampeni za kupinga BBI -Ruto

Sitaendeleza kampeni za kupinga BBI -Ruto

Naibu wa Rais, William Ruto amesisitiza hataendesha kampeni ya kupinga kura ya maamuzi kupitia Mpango wa Upatanishi, BBI.

Akihutubu katika eneo la Kitum-Endebess kwenye Kaunti ya Trans Nzoia, Ruto amesema atatii uamuzi utakaotolewa na Wakenya baada ya kura ya maamuzi.

Aidha, amekariri kwamba changamoto kuu linalokumba taifa hili ni umaskini hivyo viongozi wanapaswa kuwainua wananchi hasa vijana na akina mama kiuchumi.

Aidha, ameonya kuhusu siasa za makabila.

Ameendelea kufutilia mbali kauli ya Rais Uhuru Kenyatta kwamba ni wakati wa kuwaachia watu wa makabila mengine kuwa marais nchini humu.

Wakati uo huo, wandani wake wamezidisha shutma dhidi ya viongozi wanaopanga kumtimua Naibu wa Rais mamlakani. Wamewasuta vinara wa vyama mbalimbali wakiongozwa na Rais, Uhuru Kenyatta na Kinara wa ODM, Raila Odinga kwa kwa madai ya kumtenga Ruto katika mchakato mzima wa kuifanyia katiba marekebisho. Robert Pukose na Johannah Ng'eno ni wabunge wa Endebess na Emurua Dikiir.

Share this: