×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Raila hatajiondoa katika kinyang'anyiro cha urais cha mwaka 2022 ili kumuunga mkono yeyote -Oburu

Raila hatajiondoa katika kinyang'anyiro cha urais cha mwaka 2022 ili kumuunga mkono yeyote -Oburu

Ndugu wa Kinara wa ODM Raila Odinga, Oburu Odinga amesema Raila hatamuunga yeyote kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao.

Akizungumza katika kaunti ya Bungoma, Oboru ambaye amekuwa akifikirika kutangaza msimamo wa Raila kuhusu siasa za mwaka wa 2022, amesema Raila bado yuko katika kinyang'anyiro cha urais na kwamba wakati wake wa kustaafubado haujawadia.

Kauli hii inajiri wiki moja tu baada ya Odinga kupuuza wito wa washirika wake katika Muungano wa NASA ambao walitaka awaunge ifikapo mwaka wa 2022.

Raila alisema hawezi kumuunga kiongozi yeyote aliyekuwa katika NASA akiwamo Kinara wa ANC Musalia Mudavadi na Kinara wa WIPER Kalonzo Musyoka, kwa madai kwamba walikwepa hafla ya kujiapisha kwake baada ya kutajwa kuwa kinyume na sheria.

Odinga alisema washirika wake walidhihirisha uogam kauli ambayo imepingwa vikali na kina Kalonzo na Mudavadi ambao wamesema kwa sasa hawahitaji kuidhinishwa na yeyote kwani wanaamini wananchi watawapigia kura.

Share this: