×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Watu 181 wameambukizwa korona katika saa 24 zilizopita

Watu 181 wameambukizwa korona katika saa 24 zilizopita

Watu mia moja themanini na mmoja zaidi wameambukizwa virusi vya korona katika kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita.

Idadi ya leo imetokana na sampuli elfu tano, mia tano sabini na saba kumaanisha kwamba viwango vya maambukizi nchini leo hii ni asilimia 3. 2 ikilinganishwa na asilimia 5. 7 ya jana.

Idadi jumla ya watu walioambukizwa korona nchini sasa imefikia elfu mia moja na tano mia sita arubaini na wanane. Kaunti ya Narobi leo hii imerekodi watu wengi zaidi ambao ni mia moja na wanne, Kiambu ishirini Busia kumi na mmoja Nakuru tisa huku Mombasa na Machakos zikirekodi watu watano, watano.

Watu engine themanini na wanane wamepona katika saa ishirni na nne silizopita na kufikisha idadai jumla kuwa themanini na sita mia sita na tisa. Miongoni mwa waliopona arubaini na sita walikuwa wamelazwa katika hospitali mbalimbali na wengien arubaini na wawili walikuwa wakihudumiwa nyumbani.

Mtu mmoja amefariki dunia kumaanisha jumla sasa ni watu elfu moja mia nane hamsini na wanne.

Wagonjwa waliolazwa kwenye hospitali mbalimbali ni mia tatu arubaini na saba na elfu moja mia nne thelathini wanahudumiwa nyumbani, huku hamsini na tisa wakiwa ICU.

Share this: