
Rais Uhuru Kenyatta ndiye Mwenyekiti mpya wa Muungano wa Mataifa ya Afrika Mashariki.
Rais Kenyatta amechukua wadhfa huo kutoka kwa Rais wa Rwanda Paul Kagame ambaye amehudumu tangu mwaka 2019.
Wakati uo huo, Peter Mutuku Mathuki wa Kenya ndiye Katibu Mkuu Mpya wa Muungano huo.
Mutuku ameeteuliwa wakati wa Kongamano la Marais wa Afrika Mashariki ambalo limefanyika leo hii na atahudumu kwa kipindi cha miaka mitano.
Mutuku anachukua wadhfa huo kutoka kwa Libérat Mfumukeko ambaye amekuwa akishikilia nafasi hiyo tangu Aprili mwaka wa 2016.
Kabla ya uteuzi wake, alihudumu kama mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Kibiashara la Afrika Mashariki.
Aidha amekuwa akihusika na utekelezaji wa biashara huru miongoni mwa mataifa ya Afrika Mashariki na kubuniwa kwa Baraza la Kibiashara la Afrika.
Awali alikuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kati ya mwaka 2012-2017.
Wakati wa kongamano hilo aidha majaji wa mahakama ya Afrika Mashariki wameapishwa hivyo kupisha shughuli ya kuanza kusikiliza kesi ambazo zilikuwa zimekwamba kutokana na ukosefu wa idadai ya kutosha ya majaji.
Share this: