
Shirika la Umoja wa Mataifa Linalowashughulikia Watoto, UNICEF imelishtumu vikali tukio la kutekwa nyara kwa wanafunzi takriban 317 wa Shule ya Upili ya Serikali ya Jangebe nchini Nigeria.
Shirika la Amnesty International tawi la Nigeria aisha limeutaja utekaji nyara wa watoto kuwa ukiukaji mkubwa wa haki za kibinadamu.
Wanafunzi hao wametekwa nyara katika mji wa Zamfara. Kamishna wa Mawasiliano katika mji wa Zamfaram Suleiman Tanau amesema kwamba kundi la watu lililojihami liliwavamia wanafunzi hao usiku wa manane wakielezwa kwamba ulikuwa wakati wa kusali lakini wakatekwa nyara na kuwekwa ndani ya magari huku wengine wakitembezwa kuelekea msituni.
Wavamizi hao walifyetua risasi hewani wakati walipowateka nyara wanafunzi hao wa Shule ya Upili ya Serikali ya Jangebe. Aidha Msemaji wa Polisi nchini Nigeria, Mohammed Shehu amesema kwamba polisi kwa ushirikiano wa wanajeshi wanaendeza oparesheni ya kuwaokoa wanafunzi hao.
Mmoja wa wazazi nchini humo, Nasiru Abdullahi amesema wanawe wawili mmoja mwenye umri wa miaka kumi na mwingine kumi na mitatu ni miongoni mwa waliotekwa nyara.
Tukio hili ni la pili katika kipindi cha takirban wiki moja kwa wanafunzi kutekwa nyara. Katika kisa hicho cha awali mwanafunzi mmoja aliuliwa katika shule ya bweni kwenye eneo la Niger ambapo watu 42 walitekwa nyara wakiwamo wanafunzi 27.
Share this: