×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mwanamfalme wa Saudia, Mohamemd Bin Salman aliidhinisha maujai ya Jamal Khashoggi -Marekani

Mwanamfalme wa Saudia, Mohamemd Bin Salman aliidhinisha maujai ya Jamal Khashoggi -Marekani

Ripoti ya Ujasusi nchini Marekani imebainisha kwamba Mwanamfalme wa Saudia, Mohamemd Bin Salman aliidhinisha kuuliwa kwa mwanahabari wa taifa hilo, Jamal Khashoggi mnano mwaka 2018. Ripoti hiyo iliyotolewa na utawala wa Rais wa Marekani, Joe Biden inaoesha kwamba Bin Salman aliidhinisha kunaswa kwa Khashoggi na hata kuuliwa.

Kutokana na hali hiyo, Marekani imeweka vikwazo mbalimbali dhidi ya raia wa Saudia japo Bin Salman hajawekewa vikwazo vya moja kwa moja. Saudi Arabia hata hivyo imeipinga vikali ripoti hiyo ikisema ilikuwa ya uongo na yenye nia ya kuharibu sifa ya taifa hilo.

Khashoggi aliuliwa alipokuwa alielekea katika ubalozi wa Saudia katika eneo la Istanbul, Uturuki na mwili wake kukatwa vipande vipande japo mwili huo haukuwahi kupatikana. Mwanahabari huyo aliyeuliwa akiwa na umri wa miaka 59 kwa wakati mmoja alikuwa mshauri wa serikali ya Saudia vilevile mwanadani wa karibu wa familia ya Bin Salman japo alitofautiana nayo na kutorokea nchini Marekani mwaka 2017.

Akiwa nchini humo, mwanahabari huyo alichapisha taarifa za kushtumu uongozi wa mwanamfalme Mohammed wa Saudia hali inayodaiwa kuzidisha uhasama kati yao. 

Share this: