×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Raila ahudhuria mazishi ya Oroo Oyioka

Raila ahudhuria mazishi ya Oroo Oyioka

Kinara wa ODM Raila Odinga amewapongeza wawakilishi wadi wa eneo la Nyanza na hasa Kisii kwa kupitisha Mswada wa Marekebisho ya Katiba wa mwaka 2020. Akizungumza katika mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Bonchari John Oroo Oyioka.

Raila amewasuta wale wanapinga mchakato wa BBI  kwa kutoelewa manufaa yake kwa sekta ya jamii na katika kuwaunganisha Wakenya huku akipinga dhana kwamba ni mwanya wake wa kuingia Ikulu. Kadhalika amesisitiza kwamba eneo la Kisii litapata eneobunge jipya japo halikujumuishwa katika BBI.

Wabunge kadhaa wamehudhuria mazishi hayo wakiwamo Simba Arati na Sylvanus Osoro ambao walipata rekodi mbaya baada ya kushambuliana katika mazishi ya babaye Naibu Gavana wa Kisii. Hata hivyo leo wameonekana kuchukua mkondo mpya katika kauli zao huku Osoro akitumia fursa hiyo kusisitiza kuwa haungi mkono BBI.

 

John Oroo Oyiko ameombolezwa kwa kufanikisha maendeleo mengi katika kipindi kifupi alichohudumu huku baadhi ya viongozi wakimtaka mkewe Teresa Oroo kuchukua wadhfa wake.

Share this: