×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mswada wa BBI utashughulikiwa haraka

Mswada wa BBI utashughulikiwa haraka

Spika wa Seneti Ken Lusaka amesema ana imani kwamba mabunge yote mawili yataushughulikia Mswada wa Marekebisho ya Katiba wa mwaka 2020, chini ya kipindi cha siku sitini.

Lusaka amesema mabunge hayo tayari yamebuni kamati maalum na mjadala utaanza juma lijalo, huku akisema mabunge hayo mawili yatauidhinisha.

Ikumbukwe uongozi wa mabunge hayo utakutana mapema wiki ijayo kupanga mikakati kuhusu jinsi mswada huo utakavyoshughulikiwa.

Aidha kampeni za kuhamasisha umma zinatarajiwa kuanza Machi Mosi huku viongozi wanaopigia debe mpango mzima wa BBI wakitarajiwa kukutana na wabunge pamoja na wawakilishi wadi Machi tarehe 9 kujadili mwelekeo zaidi. Mkutano wa viongozi huo utafanywa sambamba na maadhimisho ya miezi mitatau tangu Rais Uhuru kenyatta na Kiongozi wa ODM Raila Odinga kusalimiana na kukubali kushirikiana.

Share this: