×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

KICD kufanikisha CBC kwa gredi ya tano

KICD kufanikisha CBC kwa gredi ya tano

Taasisi ya Kukuza Mitalaa, KICD tayari imeweka mikakati ya kufanikisha utekelezaji wa masomo ya gredi ya tano mwaka huu baada ya kufanikisha mafunzo ya gredi ya nne.

Akieleza haja ya washikadau katika sekta ya elimu kuendelea kushirikiana katika kufanikisha Mtalaa wa Umilisi CBC, Naibu Mkurugenzi wa KICD Patrick Andika amesema juhudi zimewekwa ili kuhakikisha mwongozo mpya wa utekelezaji wa mtalaa huo unatekelezwa baada ya kuzinduliwa na Rais Uhuru Kenyatta wiki mbili zilizopita.

Kuhusu mitihani ya kitaifa KCPE na KCSE iliyoratibiwa kufanywa mwezi ujao, Andika amesema ana imani kwamba watahiniwa wa darasa la nane na wenzao wa kidato cha nne wamejiandaa ipasavya licha ya changamoto za Janga la Korona.

Wakati uo huo, amesema KICD inalenga kufanya kampeni ya kuwahamasisha wazazi kuhusu jinsi ya kudumisha maadili miongoni mwa watoto katika jamii kufuatia visa vya utovu wa nidhamu ambavyo vimekuwa vikiripotiwa siku za hivi karibuni.

Share this: