
Mtoto mchanga anayeaminika kuwa wa siku moja anaendelea kutibiwa katika Hospitali ya Kangundo Level 4 kwenye Kaunti ya Machakos baada ya kupatikana amewekwa ndani ya gunia kisha akawekwa mtini kando ya barabara kwenye kijiji cha Matetani.
Chifu wa kijiji hicho Bethwel King'ele amesema mwanamke aliyemsikia mtoto huyo akilia alimwarifu ambapo alimwokoa.
Kwa sasa uchunguzi unaendelea kumtafuta mama aliyemwacha mwanawe hapo siku moja baada ya kujifungua, huku akionya kwamba ataadhibiwa iwapo atapatikana.
Share this: