
Na Mate Tongola,
NAIROBI, KENYA, Watu 8 wamefariki dunia kutokana na makali ya ugonjwa wa Covid-19 chini ya kipindi cha saa 24 na hivyo kufikisha 1,847 idadi ya waliofariki dunia.
Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Afya, wagonjwa wengine 119 wameripotiwa kupona, 79 miongoni mwao wakiwa waliokuwa wakitibiwa nyumbani huku waliosalia wakiwa waliokuwa hospitalini.
Idadi ya maambukizi imesalia zaidi ya watu 150 wiki hii, takwimu za leo zikibainisha kwamba watu 227 wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya korona kutokana na sampuli 4,599 zilizokusanywa na kupimwa chini ya saa 24 zilizopita.
Kiwango cha maambukizi ni asilimia 6.0.
Share this: