×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Uozo katika KEMSA wadhihirika

Uozo katika KEMSA wadhihirika

Na Beatrice Maganga,

NAIROBI, KENYA, Imebainika kwamba mojawapo ya kampuni zilizopewa zabuni ya kusambaza vifaa vya kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya korona na Mamlaka ya Usambazaji wa Dawa KEMSA ilikuwa imesajiliwa miezi miwili tu kabla ya kupata zabuni hiyo.

Kampuni ya  Shop N Buy ilisajiliwa tarehe 14 Februari mwaka jana na ikapewa zabuni ya shilingi bilioni moja kusambaza vifaa hivyo zikiwamo maski aina ya KN95. Kampuni hiyo  pia ilisambaza vifaa hivyo kwa kampuni ya Benneta Ventures, Udumart Enterprises na Trade Shop ambazo baadaye zilisambazia KEMSA kwa gharama ya juu.

Wakati uo uo, ripoti ya Mamlaka ya Ukusanyaji Kodi KRA iliyowasilishwa mbele ya Kamati ya Bunge la Kitaifa ya Uhasibu inanoesha kwamba Shop N Buy hailipi kodi ya kila mwezi. 

Kamishna Mkuu wa KRA, Githii Mburu ameiambia kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Mvita, Abdulswamad Nassir kwamba kampuni hiyo ilionesha iliagiza vifaa vya thamani ya shilingi milioni kumi pekee wala si zaidi ya bilioni mia moja. 

Kampuni hiyo ililipa kodi ya shilingi elfu mia sita themanini na saba licha ya kwamba iliagiza bidhaa nyingi  kutoka Uchina.

Mkurugenzi wa kampuni hiyo James Cheluley alikabiliwa na wakati mgumu kujibu maswali ya wanakamati wa PIC waliotaka kufahamu iwapo kuna watu wenye ushawishi waliomsaidia kupata zabuni ya KEMSA.

Awali kamati hiyo ilielezwa na aliyekuwa mkurugenzi wa mauzo katika KEMSA Charles Juma kuhusu jinsi walivyoshurutishwa na aliyekuwa Mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo Jonah Manjari kuandika barua ya kuidhinisha zabuni ya kampuni hiyo.

PIC sasa imempa Cheluley siku tatu kuwasilisha taarifa zaidi na orodha ya majina ya watu waliomsaidia kupata tenda hiyo.

Share this: