
Na Caren Omae,
NAIROBI, KENYA, Rais Uhuru Kenyatta ameliteua jopo la wanachama tisa katika Tume ya Huduma za Walimu TSC.
Kupitia notisi katika Gazeti Rasmi la Serikali, Kenyatta amesema jopo hilo limepewa jukumu la kuwachuja watahiniwa wa wadhifa wa Mwenyekiti wa TSC na mwanachama mmoja wa tume hiyo.
Jopo hilo linajumuisha Dakat Mary Gaturu, Charles Mutinda, Njoki Kahiga, Margaret Lilan Geno na Richard Kibagendi. Wengine ni Dakat Hellen Misenda, Eva Nyoike na Prof Stanley Waudo.
Ikumbukwe kwamba hatamu ya Mwenyekiti wa TSC Lydia Nzomo ilikamilika Novemba 18 mwaka uliopita.
Share this: