×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mabunge 41 yameupitisha Mswada wa BBI

Mabunge 41 yameupitisha Mswada wa BBI

Takribani Mabunge ya Kaunti 41 yameupitisha Mswada wa Marekebisho ya Katiba ya Mwaka wa  2020 huku ya Turkana, Wajir na Kericho zikiwa za hivi punde.

Baada ya kaunti 28 hapo jana kupitisha Mswada wa BBI siku iliyopewa jina Super Tuesday, leo hii mabunge ya Turkana, Wajir na Kericho yameupitisha mswada huo na sasa kufikisha 41 idadi jumla.

Katika Bunge la Kaunti ya Kericho wawakilishi wadi wameonesha hisia mseto kuhusu mswada huo huku wanaounga mkono wakiwazidi wapinzani wao wakati wa kupiga kura.

Aidha, katika Bunge la Kaunti ya Wajir, Gavana Mohamed Mahamud amelipongeza bunge kwa kupitishwa mswada huo akisema kwamba msukumo umekuwa nyongeza ya mgao wa fedha za kaunti na kubuniwa kwa Hazina ya Maendeleo ya Wadi.

Katika Kaunti ya Turkana,  wawakilishi wote waliuunga mkono. Erastus Lokaale ni Spika wa Bunge la Turkana.

Mabunge matano yanayosubiriwa kuujadili mswada huo ni Mandera, Kilifi, Uasin Gishu, Nandi na Elgeyo Marakwet.

 

Hayo yakijiri,

Jaji wa Mahakama Kuu, Justus Momanyi amewaagiza maspika wa Bunge la Kitaifa na Seneti kutochukua hatua zozote kwanza baada ya Kaunti ya Baringo kuuangusha Mswada wa Marekebisho ya Katiba wa Mwaka 2020. 

Jaji Momanyi amesema ataielekeza kesi hiyo kwa Kaimu Jaji Mkuu, Philomena Mwilu kubuni jopo la watu watatu au watano kusikiliza kesi iliyowasilishwa na wawakilishi wadi watatu wa Baringo na wakazi watatu wa kaunti hiyo kupinga namna kura ilivyofanyika na hata mswada kuangushwa.

Wakati uo huo,

Kamati ya Kiufundi ya BBI imetangaza rasmi kwamba wiki ijayo itaanza kampeni za kuupigia debe mchakato wa kufanyika kwa kura ya maaamuzi kupitia BBI.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Junet Mohammed amesema watabuni kamati za kuongoza kampeini hizo kote nchini.

Kampeini hizo zitaanza Machi tarehe mosi huku kamati kumi zikibuniwa kufanikisha mpango huo.

Kwingineko,

Wakili Charles Kanjama, ameelekea mahakamani kupinga mchakato wa kuthibitisha saini za kufanikisha kura ya maamuzi na kuwasilishwa kwa mswada wa marekebisho ya katiba kwenye kaunti.

Jaji Jairus Ngaah amemwagiza kuwasilisha stakabadhi za ombi hilo kwa wahusika wa kesi hiyo kabla ya kesho. IEBC siku ya Jumatatu ilitangaza kuthibitisha jumla ya saini milini 3.18 za BBI miongoni mwa milioni 4.3 zilizowasilishwa kwake na Kamati ya BBI.

Share this: