×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Hatimaye wauguzi wasitisha mgomo wao

Hatimaye wauguzi wasitisha mgomo wao

Hatimaye mgomo wa wauguzi umefutuliwa mbali baada ya kudumu kwa takriban siku 79. Akitoa tangazo hilo, Katibu Mkuu wa Chama cha Wauguzi nchini, KNUN Seth Panyako amewaagiza waugizi wote kurejea kazini mara moja. Panyako amesema kwamba uamuzi wa kusitisha mgomo huo umefuatia mwafaka baina ya wauguzi na kaunti kadhaa.

Hata hivyo,  amesema bado maafikiano hayajapatikana baina yao na kaunti kumi zikiwamo Nakuru, Busia, Vihiga, Kisii, Taita Taveta na Lamu japo ameelezea matumaini kwamba suluhu itapatikana hivi karibuni.

Panyako aidha ameshtumu vikali kufurushwa kwa baadhi ya wauguzi katika nyumba za kaunti baada ya kugoma akisema Chama cha KNUN kitahakikisha wanapata haki. Ikumbukwe Kaunti ya Taita Taveta ni miongoni mwa ambazo ziliwafurusha wauguzi kutoka kwenye makazi yao.

Siku ya Jumatatu, Jaji wa Mahakama ya Uajiri na Leba, Maurine Onyango aliagiza wauguzi wote kurejea kazini la sivyo wachukuliwe hatua za kinidhamu.

 Mgomo wa wauguzi uling'oa nanga Disemba 7 mwaka uliopita wakilalamikia kutolipwa mishahara kwa miezi kadhaa, kushinikiza kukabidhiwa vifaa salama vya kujikinga dhidi ya maambuzi ya virusi vya korona miongoni mwa mahitaji mengine.

Share this: