×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Kesi dhidi ya Gavana wa Migori, Okoth Obado itasikizwa jijini Nairobi

Kesi dhidi ya Gavana wa Migori, Okoth Obado itasikizwa jijini Nairobi

Kesi ya ufisadi dhidi ya Gavana wa Migori, Okoth Obado na washukiwa wengine itasikilizwa katika Mahakama ya Milimani, jijini Nairobi. Jaji James Wakiaga amelipinga ombi la kutaka kesi hiyo ihamishiwe kwenye Mahakama ya Migori.

Ombi hilo lilikuwa limewasilishwa na mmoja wa washtakiwa huku Jaji Wakiaga akisema hatua ya ombi hilo kuwasilishwa na mtu mmoja pekee ni ishara kwamba washtakiwa wengine wanataka isikilizwe Nairobi. Gavana Obado pamoja na washukiwa wengine 10  wanakabiliwa na kesi ya ufisadi wa shilingi milioni 73.

Kulingana na Ofisi ya Mkuu wa Mashtaka ya Umma, ODPP washukiwa hao pamoja na kampuni 13 zilitumika kuiba fedha za Kaunti ya Migori. Watoto wanne wa Obado wanadaiwa kunufaika na sehemu ya fedha hizo.  

Share this: