×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

kupitisha Mswada wa Marekebisho ya Katiba wa 2020 kunamaanisha nini kwa Naibu wa Rais

kupitisha Mswada wa Marekebisho ya Katiba wa 2020 kunamaanisha nini kwa Naibu wa Rais

Siku moja baada ya mabunge ya kaunti 26 kupitisha Mswada wa Marekebisho ya Katiba wa 2020 na kufikisha 38 idadi ya kaunti zilizopitisha mswada huo, wengi wanajiuliza hatua hiyo inamaanisha nini kwa Naibu wa Rais, William Ruto na wafuasi wa mrengo wa Tangatanga. Je, umaarufu wake unadidimia na utaathiri matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2022 Je, kuna uwezekano wa kubuniwa kwa mrengo imara kama ule wa Rainbow Coalition kwa wanaopinga BBI

Kinara wa ODM, Raila Odinga, mmoja wa waanzilisha wa mchakato huo tayari amewapongeza wawakilishi wadi wa mabunge yaliyopitisha. Raila amesema hatua hiyo imerahisisha pakubwa mchakato wa kuifanyia katiba marekebisho huku Kamati ya BBI ikisisitiza kwamba kura ya maamuzi itafanyika mwezi Juni mwaka huu.

Katika mtandao wake wa twitter Odinga amechapisha kimafumbo kuendelea kwa mikakati ya kupitisha BBI.

Nikinukuu, "I woke up to Busy Signal’s- REGGAE MUSIC AGAIN HIT.. “Peace and love for every day” What are you listening to"

Wimbo huo unaashiria kuendelea kwa msemo ambao wametumia tangu kuanza kwa kampeni za BBI "Nobody can stop Reggae."

Odinga anasema sasa ni dhahiri kwamba wawakilishi wadi wanafahamu vyema umuhimu wa BBI licha ya propaganda kuenezwa kuhusu mswada huo. Swali ni wawakilishi wamefahamu vyema au wameupitisha tu kufuatia motisha ya ruzuku ya magari waliyoahidiwa

Wakili na mchanganuzi wa masuala ya siasa, Martin Oloo anaeleza kile uamuzi huu unamaanisha nini kwa Naibu wa Rias William Ruto.

"Kwa wanaopinga mswada huo, itabidi warudi kwenye meza waanze kujifikiria upya kwani furaha yao ingekuwa kama mabunge haya hayangepitisha lakini sasa yamepitisha mswada huo,"asema Oloo

Ikumbukwe siku chache zilizopita matamshi ya Seneta wa Elgeyo Markwet, Kipchumba Murkomen kwamba mswada huo ukipitishwa basi baadaye wataifanyia tena katiba marekebisho kuondoa baadhi ya mambo yatayayokuwa yamepitishwa, yamezua mijadala.

"Sawa,tumieni nguvu na mpitishe mswada huo, lakini mjue kwamba tukipata fursa ya kufanya mabadiliko tutabadili yote ambayo yalipitishwa kwa kifua," asema Murkomen

Oloo anaeleza kwamba matamshi hayo ya Murkomen hayana mashiko kwani kufanya mabadiliko kutawalazimu pia kupitia kura ya maamuzi.

Vileviele Oloo anaeleza uwezakano wa kuwapo kwa mirengo mipya baada ya kura ya maamuzi.

"Watu kama Murkomen wanadhani katiba hii ni ya kuchezewa, ikumbukwe Uhuru na Raila wangekuwa na njia moja hawangepitia njia ndefu hivi, hivyo wakitaka kuibadili itabidi warudi kwa wananchi, si jambo la mzaha kwa hivyo Murkomen na wenzake waelewe,"

Miongoni mwa wanaopinga uamuzi wa mabunge ya kaunti ni mwanaharakati wa vuguvugu la Linda Katiba, Martha Karua ambaye analalamikia jinsi mswada huo ulivyopitishwa akidai wawakilishi wadi walihongwa na kwamba mapendekezo mengine hayatekelezeki.

Baadhi ya masuala yaliyowavutia wawakilishi wadi ni kuongezwa kwa mgao wa fedha za kaunti na kutengewa kwa hazina ya maendeleo katika wadi.

Share this: