×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Kaunti 37 zapitisha Mswada wa BBI

Kaunti 37 zapitisha Mswada wa BBI

Hatimaye Mabunge thelathini na saba ya kaunti yameidhinisha Mswada wa Marekebisho ya Katiba ya Mwaka wa 2020 kufuatia Mpango wa BBI,  hivyo basi kupitisha idadi ya mabunge ishirini na manne yanayohitajika kisheria ili kufanikisha kura ya maamuzi.

Mabunge ya Kaunti za Isiolo, Embu, Kwale, Kiambu na Bomet yamekuwa ya hivi punde kuupitisha mswada huo, baada ya kaunti zote za eneo la Kati ikiwamo Nyeri, Kirinyaga, Murang'a, Tharaka Nithi, Meru na Nyandarua kuupitisha awali.

Spika Stephen Ndichu alitangaza kupitishwa kwa BBI katika Bunge la Kiambu.

Kwingineko, Gavana wa Kirinyaga Ann Waiguru amesema kupitishwa kwa BBI katika eneo la Mlima Kenya ni ishara tosha kwamba wawakilishi wadi wamefahamu manufaa yake, na kwamba hawawezi kupinga msimamo wa Rais Uhuru Kenyatta.

Kauli sawa na hiyo imetolewa na Gavana wa Murang'a Mwangi wa Iria.

Hali imekuwa sawa katika eneo la Ukambani ambapo Kaunti tatu, Makueni, Kitui na Machakos kwa pamoja zimeupitisha Mswada huo.

Aidha, Mabunge ya Mombasa, Bungoma, Kakamega na Nakuru ni miongoni mwa mengine yaliyopitisha BBI leo hii.

Hata hivyo, Katika Bunge Nyandarua, kizaazaa kilizuka kabla ya mswada huo kupitishwa baada ya umeme kupotea, hivyo basi kuwalazimu wawakilishi wadi kuujadili wakiwa gizani.

Kufikia sasa ni Bunge la Baringo pekee ambalo limeangusha BBI, huku Kamati ya Kitaifa inayoshughulikia BBI ikiwa tayari imeweka mikakati ya kampeni za kura ya maamuzi.

Share this: