×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

10 Wafariki kufuatia Covid-19, 194 waambukizwa

10 Wafariki kufuatia Covid-19, 194 waambukizwa

Watu kumi zaidi wameaga dunia kutokana na ugonjwa wa Covid-19.

Idadi hii inafikisha jumla ya vifo kuwa elfu moja, mia nane thelathini na saba kote nchini.

Katika taarifa, Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema watu wengine thelathini na tisa wamepona Covid-19 na kufikisha jumla ya waliopona kuwa elfu themanini na tano, mia sita sitini na watano.

Wakati uo huo, watu mia moja tisini na wanne wamethibitishwa kuambukizwa Korona kutokana na sampuli elfu tatu, mia tisa thelathini na tano zilizopimwa katika kipindi cha saa 24 zilizopita.

Kwa sasa idadi ya maambukizi imefikia watu elfu mia moja na nne na mia tano kote nchini.

Viwango vya maambukzii leo hii ni asilimia 5 kulinganishwa na asilimia 3 ya jana.

Share this: