×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mgomo wa Kitaifa wa Matabibu umefikia kikoma

Mgomo wa Kitaifa wa Matabibu umefikia kikoma

Hatimaye Mgomo wa Kitaifa wa Matabibu umefikia kikomo leo.

Chama cha Matabibu Nchini KUCO kimesitisha rasmi mgomo wake kufuatia agizo la Jaji wa Mahakama ya Leba Maureen Onyango.

Mgomo huo umedumu kwa zaidi ya siku sabini na kuathiri pakubwa utoaji wa huduma za matibabu kwa Wakenya hasa wakati huu wa Janga la Korona.

Licha ya kuwaagiza matabibu wote kurejea kazini,  Mwenyekiti wa KUCO, Peter Wachira amesema matakwa yao bado hayajatekelezwa na serikali.

Mwenyekiti huyo amesema matatizo yanayokumba sekta ya afya nchini yanatokana na ukosefu wa Tume ya Kitaifa ya Afya ambayo imengeshughulikia malalamiko yao.

Aidha amesema wahudumu wengi wa afya wamefariki dunia kutokana na mazingira dunia ya kufanyia kazi na ukosefu wa vifaa vya kujikinga dhidi ya maambukizi ya korona.

Share this: