×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Wabunge waomboleza kifo cha Wakapee

Wabunge waomboleza kifo cha Wakapee

Wabunge wametumia vikao vya leo alasiri kutuma risala za rambirambi kwa familia ya Mbunge wa Juja, Francis Munyua Waititu maarufu Wakapee aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo.

Wabunge hao mmoja baada ya mwingine wamemmiminia sifa mbunge huyo aliyefariki kutokana na saratani ya ubongo.

Wamemtaja Wakapee kuwa kiongozi aliyejitolea kuhakikisha wakazi wa eneo lake wananufaika na miradi ya maendeleo. Pia wamemkumbuka kwa kuwahamasisha wananchi kuhusu ugonjwa wa saratani.

Kwa upande wake, Mbunge wa Rarieda Otiende Amollo, amesikitishwa na jinsi ugonjwa wa saratani unazidi kuwaangamiza watu nchini.

Akitoa mfano wa Kaunti ya Siaya, Amollo amesema miongoni mwa watu kumi, watatu au wanne wanaugua ugonjwa huo.

Ameitaka serikali kufanya kipaumbele afya ya Wakenya.

Wakapee aliwahi kufichua kwa vyombo vya habari kwamba idadi ya wabunge wanaoelekea nchini India kwa matibabu ya saratani ilikuwa ya juu zaidi na mwaka huo 2018, kuthibitishwa kwamba wabunge zaidi ya 10 walikuwa wakiugua saratani. Dadaye pia alifariki dunia kutokana na saratani.

Share this: