×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mkurugenzi asambaza bidhaa za KEMSA mitandaoni!

Mkurugenzi asambaza bidhaa za KEMSA mitandaoni!

Mkurugenzi wa Kampuni Moja inayohusishwa na wizi wa fedha za Vifaa vya Kukabili Mambukizi ya Virusi vya Korona katika Mamlaka ya Kusambaza Vifaa vya Matibabu KEMSA, ameshangaza Kamati ya Afya Bungeni baada ya kusimulia jinsi alivyosambaza vifaa hivyo kupitia mitandao ya kijamii.

Joel Ndegwa, ambaye ni Meneja Mkurugenzi wa Kampuni ya Meldian Enterprises Limited, amesema alikuwa na mpango wa kusambaza vifaa hivyo kwa KEMSA kuaznia mwezi Januari mwaka huu kwa kutumia biashara za mtandaoni.

Kampuni ya Ndegwa ilikuwa imepata tenda ya shilingi milioni mia mbili na ishirini na tano ili kusambaza vifaa vya kudhibi Korona.

Amesema kufikia sasa amelipwa shilingi milioni mia moja na kumi na saba pekee.

Hata hivyo, wanachama wa  Kamati ya Uwekezeji wa Umma wamemtaka Ndegwa kueleza jinsi kampuni yake ilivyosambaza vifaa hivyo kwa KEMSA, ibaada ya kushindwa kutoa stakabadhi za kuoesha namna alivyofanya.

Juma lililopita, Zubeda Nyamlondo Ngobi, ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Aszure Commercial Services aliwashangaza wanachama wa kamati hiyo baada ya kusimuliwa jinsi alivyopata tenda ya shilingi milioni mia tatu ya KEMSA.

Share this: