×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mabunge ya Kaunti yapongezwa kwa kupitisha BBI

Mabunge ya Kaunti yapongezwa kwa kupitisha BBI

Aliyekuwa kamishna wa Tume ya Uchaguzi IEBC awali ikiitwa ECK Balozi Jack Tumwa, ameyapongeza mabunge ya kaunti ambayo yamepitisha mswada wa marekebisho ya katiba wa 2020 akiutaja mswada huo kuwa chanzo cha kuboresha mfumo wa ugatuzi nchini.

Akizungumza muda mfupi tu baada ya Bunge la Bungoma kupitisha mswada huo, Tumwa amesema kilichosalia sasa ni kufanya uhamasisho kwa Wakenya ili kufahamu yaliyomo kwenye mswada huo.

Kauli sawa na hiyo imetolewa na aliyekuwa diwani wa Wadi ya Bokoli John Wambalaba akisema ipo haja ya nakala za BBI kusambazwa mashinani kabla ya kura ya maamuzi ili kuwaruhusu Wakenya kujisomea na kufanya maamuzi ya busara.

Share this: