
Ni wazi kwamba kura ya maamuzi itafanyika.
Aidha, Mswada wa 2020 wa Marekebisho ya Katiba unatoa mwanya wa ubabe wa kisiasa kudhihirika humu nchini, Naibu wa Rais William Ruto na Kinara wa ODM Raila Odinga wakiwekwa kwenye mizani.
Mchanganuzi wa masuala ya kisiasa, Javas Bigambo anasema kuwa kupitishwa kwa mswada huo kunamweka Odinga kifua mbele hasa ikizingatiwa amekuwa akipigania marekebisho ya katiba.
Je, kupitishwa kwa mswada huu kunamaanisha nini kwa Naibu wa Rais
Hata hivyo, mchambuzi mwenza ambaye ni Mhadhiri, Philip Chebunet anatofautiana na kauli hiyo huku akisema hatua ya Ruto kukosa kutoa msimamo kuhusu mswada huo ni kutokana na azma yake ya kulenga urais mwaka wa 2022.
Share this: