×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Kaunti 29 zapitisha Mswada wa BBI

Kaunti 29 zapitisha Mswada wa BBI

Mabunge 29 yamepitisha Mswada wa Marekebisho ya Katiba na kupitisha idadai ya mabunge 24 yanayohitajika kikatiba huku Kaunti ya Nakuru ikiwa ya hivi punde zaidi ambapo wawakilishi wadi 62 wameunga na 11 kupinga.

Kaunti zote za eneo la kati ambazo Nyeri, Kirinyaga, Muranga na Nyandarua  pia zimekuwa kupitisha baada ya mabunge ya kaunti hizo muda mfupi uliopita kwa pamoja  kupiga kura ya kuunga. Katika Kaunti yaMurang'a wawakilishi pamoja na Gavana Mwangi wa Iria waliamua kucheza 'Firirinda' kidogo kwa furaha.

Katika Kaunti ya Kirinyaga, Anne Waiguru amesisitiza kuwa jamii ya Mlima Kenya haiwezi kuhongwa kwenda kinyume na mahitaji yake.

Kwenye Kaunti ya Nyeri, wawakilishi wadi arubaini na wawili wameunga mkono msaada huo huku wawakilishi wawili Kiruga Thuku wa Chinga na mwenzake wa Eric Wamumbi Konyu wakipinga.

Mswada huo pia umepita katika Kaunti za Tharaka Nithi na Meru.  

Share this: