×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Sipingi ruzuku kwa wawakilishi wadi bali nahitaji ufafanuzi, asema Nyakango

Sipingi ruzuku kwa wawakilishi wadi bali nahitaji ufafanuzi, asema Nyakango

Ofisi ya Mkuu wa Bajeti imejitenga na madai kwamba inapinga wawakilishi wadi kupata ruzuku ya magari kufuatia taarifa yake ya awali kuhusu suala hilo.

Katika barua ya awali, Msimamizi wa Bajeti Margaret Nyakang'o alikuwa ameomba ufafanuzi wa jinsi ya kutekeleza ruzuku ikizingatiwa wawakilishi wadi wengi tayari walikuwa wamechukua mikopo ya magari na walikuwa katika atua mbalimbali za kuilipa.

Barua hiyo iliibua hisia kwamba ofisi hiyo ni kizingiti katika mchakato mzima.

Hata hivyo, Nyakang'o amesisitiza kuwa jukumu lake ni kuidhinisha bajeti baada ya kutosheka  kwamba sheria imetimizwa.

Kadhalika amesisitiza hana mamlaka ya kukiuka umauzi uloochukuliwa na Tume ya Kuratibu Mishahara ya Wafanyakazi wa Umma. Wawakilishi wadi wanatarajiwa kupata ruzuku ya shilingi milioni 2 ili kununua magari.

Share this: