×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Kurutu azimia na kufariki dunia huko Bungoma

Kurutu azimia na kufariki dunia huko Bungoma

Biwi la simanzi limetanda katika Kijiji cha Bokoli kwenye Kaunti ya Bungoma kufuatia kifo cha mvulana, ambacho kimetokea wakati wa shughuli ya usajili wa makurutu wa kujiunga na kikosi cha polisi.

Dennis Mukhebi amezimia katika Uwanja wa Shule ya Upili ya Bokoli wakati wa kufanya mazoezi kabla ya kutangazwa kufariki dunia alipofikishwa hospitali.

Marehemu alikuwa tayari amekamilisha mchujo wote kabla ya kuzimia.

Naibu Kamanda wa Polisi wa eneo hilo, Dennis Ng'etich amesema juhudi za madaktari kumwokoa hazikufua dafu. Wakati wa shughuli hiyo, vijana kumi na wawili walisajiliwa kujiunga na kikosi cha polisi.

Kwenye Kaunti ya Mombasa, mchungaji amelazimika kumfanyia maombi ya dharura kijana mmoja aliyekuwa amejitokeza kwa shughuli iyo hiyo, alipoanza kuwapiga wenzake muda mfupi baada ya kumaliza kukimbia.

Iliwalazimu polisi kumkamata huku mchungaji akimwombea.

Sababu za mwanamume huyo kutatiza shughuli hiyo hazijaabainika

Share this: