×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Odinga amkashifu mkaguzi wa bajeti kuhusu ruzuku ya magari

Odinga amkashifu mkaguzi wa bajeti kuhusu ruzuku ya magari

Kinara wa ODM Raila Odinga ameikosoa Ofisi ya Mdhibiti wa Bajeti ya Serikali kufuatia kauli yake kwamba ruzuku kwa wawakilishi wadi waliyoahuidiwa na Rais Uhuru Kenyatta haikujumuishwa kwenye bajeti, na hivyo basi huenda ikawalazimu kusburi kwa muda.

Katika taarifa yake kwenye vyombo vya habari, Odinga aidha amesema ruzuku hiyo ni haki ya wawakilishi wadi kupewa na wala si suala la iwapo imejumuishwa kwenye bajeti au la.

Aidha ameikosoa ofisi hiyo, akisema jukumu lake kuu ni kufuatilia jinsi bajeti ya serikali ya kitaifa vilevile zile za kaunti zinavyotekelezwa na wala si kuamua jinsi bajeti hiyo inavyotumika.

Katika barua hiyo ndefu, Odinga ameongeza kuwa uamuzi unaofanywa na Rais kuhusu bajeti hauwezi kubatilishwa na afisa yeyote yule na kwamba Kauli ya Mdhibiti wa Bajeti ya Serikali Magret Nyakango ni ya kushangaza.

Ameitaja ofisi hiyo kama adui wa maendeleo mashinani.

Hayo yanajiri huku Ofisi ya Mdhibiti wa Bajeti ikiiandikia Tume ya Kuratibu Mishahara ya Wafanyakazi wa Umma, SRC ikitaka ushauri wa jinsi agizo la Rais la ruzuku ya magari kwa wawakilishi wadi litakavyotekelezwa.

Kufikia Jumatano wiki jana, SRC ilithibitisha kupokea maombi mengi kutoka kwa serikali za kaunti ya kutaka kutekelezwa kwa agizo la Rais ili kuhakikisha kuwa wawakilishi wadi vilevile maspika wa mabunge ya kaunti wanapata ruzuku hiyo.

Share this: