×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×
Samburu yapitisha BBI

Kaunti ya Samburu imekuwa ya kumi na mbili kuupitisha Mswada wa Marekebisho ya Katiba ya Mwaka wa 2020.

Wawakilishi wote ishirini na sita wamepiga kura ya kuupitisha mswada huo.

Tayari kaunti kumi na moja zimepitisha mswada wenyewe.

Kaunti hizo ni Siaya, Kisumu, Homa Bay, Kisii, Laikipia, Busia, Trans Nzoia, Nairobi, Kajiado na Pokot Magharibi.

Hata hivyo, Kaunti ya Baringo iliangusha mswada huo.

Wakati uo huo, kaunti zaidi ya kumi zinatarajiwa kuupitisha mswada huo wakati wa vikao vya Jumanne yaani Super Tuesday.

Kaunti hizo ni Migori, Nyeri, Kirinyaga, Meru, Makueni, Machakos, Kitui, Nyamira, Kilifi, Mombasa, Taita Taveta, Lamu, Isiolo, Garissa, Isiolo, Bungoma na Nakuru.

Tayari Seneta wa Bungoma, Moses Wetangula amethibitisha kwamba wawakilishi wadi wa kaunti hiyo watapitisha mswada huo baada ya mkutano wa leo mjini Bungoma.

Aidha, wawakilishi wadi wa eneo la Ukambani wameafikiana kuupitisha baada ya kufanya mkutano na magavana.

Share this: