×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Ruto atatea kauli mbiu ya Hustler Nation

Ruto atatea kauli mbiu ya Hustler Nation

Naibu wa Rais William Ruto ameutetea mpango wake wa kuwawezesha akina mama na vijana mashinani akisema unalenga kuisaidia serikali kulipa madeni kupitia ushuru utakaotozwa.

Akiwahutubia waombolezaji katika hafla ya mazishi kwenye Kaunti ya Uasin Gishu, Ruto amesisitiza kwamba mpango huo unalenga kuwawezesha Wakenya kujiajiri wenyewe na kuchangia moja kwa moja katika uchumi wa taifa.

Wakati uo huo amewahakikishia Wakenya kwamba changamoto zinazoikumba serikali ya Jubilee zitatatuliwe ili kuhakikisha kwamba taifa linadumisha utangamano.

Aidha amewataka viongozi waliochanguliwa vilevile maafisa wakuu serikalini kuyatekeleza majukumu yao ipasavyo. Ameonya dhidi ya siasa za chuki na ukabila ambazo zimekuwa zikiendelezwa na viongozi, akiwashauri Wakenya kuwapuuza.

Ikumbukwe Tume ya Kitaifa na Uwiano NCIC nayo ilitoa wito huo wa kusitishwa kwa cheche za maneno baina ya viongozi ili kuhakikisha amani inadumishwa nchini.

Share this: