×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Viongozi wa Ukambani wasema watapitisha BBI

Viongozi wa Ukambani wasema watapitisha BBI

Viongozi wa eneo la Kiuchumi la Kusini Kaskazini mwa Nchi South Eastern Kenya Economic Block SEKEB, wameafikiana kwa kauli moja kupitisha Mswada wa Marekebisho ya Katiba ya Mwaka wa 2020 kesho Jumanne.

Magavana wa Kaunti za Machakos , Kitui, Makueni na wawakilishi wadi zaidi ya sitini wamekongamana mapema leo na kuafikia uamuzi huo.

Wakizungumza baaada ya mkutano huo Magavana,Dakta  Alfred Mutua na Profesa Kivutha Kibwana wamesema kwamba uamuzi huo umeafikiwa kufuatia vikao vya umma ambapo wananchi wameshirikishwa kikamilifu.

Aidha wamesema kwamba wananchi wameamua kuunga mkono BBI kutokana na mapendekezo ya kuongeza mgao wa fedha kwa kaunti na kubuniwa kwa hazina ya wadi.

Viongozi hao aidha wamesema wataendelea kufanya kipau mbele maslahi ya wananchi wa eneo la Ukambani huku wakiwakashifu vikali wanaopinga mchakato huo.

Ikumbukwe kwamba awali palikuwa na suitafahamu miongoni mwa viongozi wa Ukambani kuhusu BBI, wandani wa Gavana Mutua wakisema baadhi ya mapendekezo katika BBI yanahujumu azma yake ya kuwa rais.

Adha huko Makueni kulikuwa na mgawanyiko kuhusu BBI miongoni mwa viongozina wananchi suala ambalo limetatuliwa kwa sasa.

Share this: