×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Watu 105 waambukizwa korona huku 4 wakifariki dunia

Watu 105 waambukizwa korona huku 4 wakifariki dunia

Watu mia moja na watano wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya korona kutokana na sampuli elfu tatu, mia tano sabini na tatu zilizopimwa katika kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita.

Takwimu za leo sasa zinafikisha jumla ya watu walioambukizwa kuwa elfu mia moja na nne, mia tatu na sita.

Kiwango cha maambukizi leo kimeshuka na kuwa asilimia 2.9 kulinganishwa na asilimia sita ya jana.

Miongoni mwa walioambukizwa themanini na wanane ni Wakenya huku kumi na saba wakiwa wa mataifa yakigeni. Aidha mtu mchanga ana umri wa miaka kumi na mmoja na mkongwe themanini na miwili.Wanaume ni sabini na wawili na wanawake ni thelathini na  watatu.

Kaunti ya Nairobi inaendelea kuongoza kwa maambukizi mapya ambapo leo watu sitini na wanane wameambukizwa ikifuatwa na Kiambu kumi na wawili.

Aidha watu arubaini na tisa wamepona korona, thelathini na wanne walikuwa wakihudumiwa nyumbani na kumi na watano hospitalini.

Hata hivyo, watu wengine wanne wamefariki dunia kutokana na Covid-19 na sasa kufikisha jumla ya watu waliofariki kuwa elfu moja,mia nane ishirini na saba.

Share this: