×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Hatukuitaji utuunge mkono 2022 -Mudavadi na Kalonzo wamwambia Raila

Hatukuitaji utuunge mkono 2022 -Mudavadi na Kalonzo wamwambia Raila

Na Carren Omae

NAIROBI, KENYA: Miezi michache tu kabla ya uchaguzi mkuu mwaka ujao, tofauti miongoni mwa vinara wa Muungano wa NASA zimeanza kujitokeza wazi.

Kinara wa Wiper, Kalonzo Musyoka na mwenzake wa ANC Musalia Mudavadi wamemshtumu vikali Raila Odinga wa ODM, kufuatia kauli kwamba hatamuunga mkono kiongozi yeyote ambaye hakuhudhuria uapisho wake mwaka wa 2022.

Kalonzo amesema hamtegemei yeyote Raila amuunge mkono katika azma yake ya kuwania urais mwaka ujao.

Kalonzo amesema hakuhudhuria shughuli ya uapisho wa Raila kwani ilikuwa kinyume cha sheria, akisema ndiye aliyemshauri kufanya mazungumzo na Rais Uhuru Kenyatta.

Kauli sawa na hiyo imetolewa na Mbunge wa Matungulu Stephen Mule.

Mudavadi anamtaka Raila kuwaambia Wakenya ukweli, akisema aliwahadaa kisha akaenda katika Bustani ya Uhuru kisiri ili kujiapisha.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari Mudavadi amesema hatua ya Odinga kujiapisha ilikuwa njama ya kutafuta mapatano na Rais Uhuru Kenyatta.


Anasema baada ya mapatano yao, Odinga amekuwa akiwatishia vinara wenza huku akisahau mchango wao walipokuwa katika Muungano wa NASA.

Kulingana na Mudavadi, Odinga ana haki ya kumuunga mkono kiongozi mwingine kando na vinara wenza na kusema hana mamlaka ya kuwazuia.

Kadhalika, kiongozi huyo amemsuta Odinga kwa kujiondoa katika marudio ya uchaguzi wa urais mwaka wa 2017, akisisitiza wataendelea kumkumbusha alipe deni la kisiasa.

Vilevile, amemtaja kuwa mlaghai wa kisiasa anayewahadaa wenzake kwa manufaa yake binafsi.

Ikumbukwe japo Raila hajatangaza wazi wapo atawania kiti cha urais kumekuwapo na shinikizo hasa kutoka kwa wafuasi wa Mudavadi wanaomtaka ajiondoe na kumuunga mkono jinsi walivyokubaliana kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2017.

Share this: