×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

6 wameaga dunia, 208 wakiambukizwa korona

6 wameaga dunia, 208 wakiambukizwa korona

Na Carren Omae

NAIROBI, KENYA: Watu sita wamefariki dunia kutokana na virusi vya korona katika saa ishirini na nne zilizopita. Idadi hii imefikisha idadi jumla ya waliofariki dunia kuwa elfu moja mia nane ishirini na watatu.

Wakati uo huo, watu wengine mia mbili na wanane wameambukizwa virusi vya korona katika kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita. Idadi hii imetokana na sampuli elfu tatu mia nne kumi na tano zilizopimwa katika kipindi hicho kimaanisha viwango vya maambukizi leo hii ni asilimia 6.

Jumla ya watu walioambukizwa korona nchini kufikia sasa ni elfu mia moja na wanne mia mbili na mmoja.

Miongoni mwa waliothibitishwa kuambukizwa Wakenya ni mia moja sabini na watatu na thelathini na wanane ni raia wa kigeni. Mia moja arubaini na saba ni wanaume na sitini na mmoja wakiwa wanawake.

Wagonjwa wengine thelathini na saba wamepona na kufikisha idadi jumla kuwa elfu themanini na tano mia tano sabini na saba.

Kwa sasa kuna wagonjwa mia tatu na wanane ambao wamelazwa katika hospitali mbalimbali huku wengine elfu moja mia moja na sitini wakiendelea kuhudumiwa nyumbani.

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema walio katika vyumba vya wagonjwa mahututi, ICU ni wagonjwa hamsini na mmoja.


 

Share this: