×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

WHO yaiagiza Tanzania kuweka wazi takwimu kuhusu korona

WHO yaiagiza Tanzania kuweka wazi takwimu kuhusu korona

Na Carren Omae

NAIROBI, KENYA: Shirika la Afya Duniani WHO limeagiza Tanzania kuanza kutangaza takwimu za maambukizi ya kila siku ya virusi vya Korona.

Katika taarifa Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus, vilevile ameagiza taifa hilo jirani kuanza kuzingatia masharti ya kudhibiti maambukizi ya virusi hivyo.

Amesema baadhi ya  Watanzania wanaosafiri kuelekea mataifa jirani wamethibitishwa kuambukizwa korona, hivyo ni muhimu kwa Tanzania kuanza kuweka wazi data kuhusu maambukizi hayo.

Ikumbukwe mara ya mwisho kwa Tanzania kuripoti idadi ya watu walioambukizwa korona ilikuwa Aprili tarehe 29 mwaka uliopota, ambapo visa vilikuwa vimefikia mia tano na tisa, ambapo waliofariki dunia walikuwa ishirini na mmoja na mia moja themanini na watatu kupona.

Baadaye Rais wa Tanzania John Magufuli aliwaongoza Watanzania kwa maombi ya siku tatu, kisha kudai kwamba korona iilukuwa imeisha kabisa nchini humo kutokana na maombi hayo.

Baada ya miezi kadhaa ya kukataa kukubali kwamba Korona ingalipo nchini humo, Ijumaa iliyopita Magufuli pia alisema ataongoza maombi ya kumaliza korona kwa siku tatu.

Hata hivyo, mataifa kadhaa duniani yametaja Tanzania kuwa taifa ambalo visa vya korona vinaongezeka zaidi, huku Marekani ikiwaonya raia wake dhidi ya kusafiri kuelekea nchini humo.

Mwezi jana pia Rais Magufuli alifutilia mbali uwezekano wa taifa lake kutumia chanjo dhidi ya korona ambazo zimepatikana kufikia sasa, akisema ndizo zinazochangia maambukizi hata zaidi.

Katika siku za hivi karibuni watu kadhaa mashuhuri wamefariki dunia nchini humo huku ikidaiwa kwamba vifo vyao vimetokana na Korona, licha ya serikali kuendelea kusalia kimya.

Leo hii, Magufuli ameonekana kubadili msimamo wake alipowashauri raia wa Tanzania kuchukua tahadhari huku akiendeleza shtuma dhidi ya mataifa anayodai yanachangia katika kuongezeka kwa virusi hivyo kwa manufaa yao ya kuichumi.

Share this: