×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Ruto asuta serikali kwa kuwahangaisha wandani wake

Ruto asuta serikali kwa kuwahangaisha wandani wake

Kizaazaa kimeshuhudiwa mapema leo katika Wadi ya London, kwenye Kaunti ya Nakuru, wakati polisi walipowarushia vitoza machozi wanasiasa wa mrengo wa Tanga Tanga waliokuwa wamefika kumpigia debe mgombea wa kiti cha wadi hiyo kwa tiketi ya UDA Antony Nzioka.

Wanasiasa hao akiwamo Seneta wa Nakuru Susan Kihika, Mbunge wa Nyali Mohamed Ali, John Kiarie wa Dagoretti Kaskazini na Cecily Mbarire ambaye ni mbunge maalum, walikabiliwa  na maafisa wa GSU katika ofisi ya UDA, kwenye eneo la Milimani Mjini Nakuru.

Haijabainika sababu kamili ya maafisa wa polisi kuzuia mkutano huo kufanyika, ila inaamika waandalizi hawakuwa wamezingatia masharti ya kudhibiti Korona.

Baadaye walifanikiwa kufanya mkutano, ambapo walitumia muda wao kumshtumu Rais Uhuru Kenyatta, Waziri wa Masuala ya Ndani ya Nchi na Usalama Dkt. Fred Matiang'i na Ispekta Mkuu wa Polisi Hillary Mutyambai kwa madai ya kuwahagaisha.

Susan Kihika ni Seneta wa Nakuru.

Wanasiasa hao aidha wameilaumu serikali wakisema ndiyo inayozua ghasia huku ikiulaumu upinzani.

Hayo yalipokuwa yakiendelea Naibu wa Rais William Ruto alipeleka siasa za Wilbaro kwenye kaunti ya Baringo.

Ruto aliongoza hafla ya kufungua kanisa Katoliki la Kituro, kabla ya kuhutubia umma kwenye maeneo mbalimbali.

Ruto pia alikashifu hatua ya wandani wake kuendelea kuhangaishwa na maafisa na idara za serikali.

Aidha amesema hatashtushwa na njama za baadhi ya watu wanaotaka aondoke serikalini.

Share this: