×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mudavadi awasihi Wakenya kumchagua kuwa rais 2022

Mudavadi awasihi Wakenya kumchagua kuwa rais 2022

Kinara wa ANC Musalia Mudavadi ameeleza haja ya Wakenya kumchagua rais ambaye atafanikisha maendeleo badala ya ushawishi wa wanasiasa binafsi.

Akizungumza baada ya kutawazwa na Wazee wa Jamii ya Abaluhyia ili kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao, katika boma lake la Mululu kwenye kaunti ya Vihiga, Mudavadi amesema yuko tayari kushirikiana na washikadau mbalimbali katika kufanikisha maendeleo.

Amesema Jamii ya Magharibi ina uwezo wa kumtoa rais iwapo viongozi wa eneo holo watashirikiana bila mwingilio kutoka maeneo mengine.

Ikumbukwe mwaka wa 2008, Wazee wa Jamii ya Abaluhyia walimtawaza Mudavadi kuwa kiongozi wa kisiasa wa jamii hiyo kwenye Bustani ya Muliro mjini Kakamega.

Hayo yamejiri huku Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho akizindua rasmi mipango yake ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao.

Akizungumza katika Kaunti ya Lamu baada ya kufanya mkutano na viongozi wa eneo la Pwani kwa ajenda ya umoja wa eneo hilo, Joho amesema wakati umefika kwa vigogo wengine wa kisiasa kumuunga mkono ifikapo mwaka wa 2022.

Mkutano wa leo umekuwa wa tatu kufanyika kwenye Kaunti ya Lamu ambapo Maseneta, Wabunge na Wawakilishi wadi pia wamehudhuria.

Haya yanajiri wakati ambapo kumekuwapo na mjadala mkali wa iwapo viongozi hao watabuni chama chao cha kisiasa ambacho watakitumia kuwania nafasi za uongozi wakati wa uchaguzi mkuu ujao au la. 

Share this: