
Watu wengine mia moja hamsini na wawili wameambukizwa Korona kutokana na sampuli elfu tatu, mia saba thelathini na nne zilizopimwa katika saa 24 zilizopita.
Idadi ya leo inafikisha watu elfu mia moja na tatu, mia tisa tisini na watatu walioambukizwa Korona kote nchini.
Miongoni mwa walioambukizwa, mia moja thelathini na saba ni Wakenya, huku raia wa kigeni wakiwa kumi na watano.
Mtoto wa miaka miwili na mkongwe wa miaka themanini na minane ni miongoni mwa walioambukizwa.
Viwango vya maambukizi leo hii ni asilimia 4.1.
Katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari, Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema watu wengine wanane wamepona Ugonjwa wa Covid-19 na kufikisha jumla ya waliopona kuwa elfu themanini na tano, mia tano arubaini.
Hata hivyo, watu wanne wamefariki dunia kutokana na COVID-19.
Kufikia sasa, idadi ya vifo kutokana na COVID-19 nchini humu imefikia elfu moja, mia nane kumi na saba.
Share this: